SOMO LA LEO

SOMO:NITASIMAMA TENA
PASTOR:PAUL JOSHUA
FROM:MWANZA
Ayubu 22:28-29 Mungu anaweza kuruhusu magumu /majaribu yakupate ili ajinyakulie utukufu mahali ambapo tumaini limekosekana.mfano Ayubu aliporomoka chini kwa magonjwa mifugo yake ilikufa, watoto wake wakafa, laikin bado alimtegemea Mungu na bado aliniinuka tena.
ukiona ndoa imevunjika ujue yupo aliyeivunja ukiona biashara yako imekwisha ujue yupo aliyeiporomosha lakini nakutangazia siku ya leo yupo Mungu asiyeshindwa na chochote atakusaidia
ayubu 30:19 Ayubu alisema wamenibwaga chini kwenye matope anajiona kama hana msaada ila Mungu yupo atakusaidia atakushindia na atakuokoa.zaburi 118:13
katika ulimwengu wa roho watu wanaweza kukaa vikao wakisema tukuangushe chini iwe kwenye biashara yako,kazi, au ndoa ila yupo Mungu ambaye njia za kuokoa zina yeye
kama Mungu alivyomwambia Daudi hatamuacha ndivyo atakavyo kuwa pamoja nawe kukusaidia naamu kukushika kwa mkono wake wa kuume wa haki yake zaburi 62:4.
kwenye neno la Mungu kuna tahadhari usimuguse masihi wa Mungu wala kumdhuru atakayefanya ivo atakuwa amegusa mboni ya jicho la Mungu na atashughulika nae.





FIND US ON.
BLOG:www.http://ufufuonauzima-mwanza.blogspot.com(visit us)
ustream:http://www.ustream.tv/channel/ufufuo-na-uzima--mwanza(follow us)
Youtube:Pastor Samson gwajima(follow us)
Facebook Page:Pastor samson gwajima(like our Page)
Twiter:Pastor Samson Gwajima




SOMO:SITATOA SADAKA KWA MASHETANI
PASTOR:MAXMILLIAN MACHUMU(MWANAMAPINDUZI)
FROM:DAR
Leo shetan atajuta kilichomtuma yeye kuwa shetan"Kumbukumbu la torati 32:17 walawi 17:7 1wakolintho 10:20 maadamu mtu anaishi ni lazima utoe iwe kwa Mungu au shetani ni lazima utoe ili ufikie baraka zako;Mungu wa duniani wapo wawili tu nao wote wanataka utoe sadaka ila Mungu Yehova anataka utoe sadaka kwa hiari ila shetan sadaka yake ni ya damu za wanadamu au wanyama,sadaka za shetan zinatolewa kwenye misiba,magonjwa ukipata pesa tu anafungulia magonjwa kwa watu wako wa karibu au misiba ili iwe isiwe utatumia pesa yako ndipo utakuwa umekuwa umetoa sadaka tayari kwa shetani,kwa njia ya sadaka; leo tumeokolewa kwasababu Mungu mwenyewe alianza kutoa sadaka ya mwanae wa pekee YESU KRISTO,ukimtolea Mungu sadaka yeye atalinda familia yako maisha yako kwa ujumla.
UKIRI:Baba katika jina la Yesu nakataa kutoa sadaka kwa mashetani siwezi kutoa tena sadaka kwa magonjwa wala misiba kwenye familia yangu niko tayari leo kutoa sadaka kwako ili nifanikiwe ili niendelee mbele nikijua Mungu utalinda kile nitakachofanya iwe biashara au kazi katika jina la Yesu,shetan umenimalizia pesa yangu nasoma kwa gharama kubwa alafu na feli leo ni mwisho sitapoteza tena, sitazulumiwa tena, sitapata ajali tena, vitu vyangu havitaharibika, watoto wangu hawataumwa tena katika jina la Yesu.


                                             PASTOR:MAXMILLIAN MACHUMU(MWANAMAPINDUZI)



SOMO:NGUVU YA UMILIKI
PASTOR: BENEDICT KAMZEE
FROM:KATAVI
mwanzo 1:27 nguvu ya kwanza ya kumiliki ni kwenye ndoa mana hapa ndo imebeba familia nzima uzao wa watoto ndo mana shetani anakimbilia ndoa kuiharibu akijua kila kitu kitaaribika joshua 3:1-5maneno yote uliyofundishwa kwenye madhabahu ya Mungu usipoyafuata kumiliki kwako hakupo ni lazima ufatilie neno la Mungu ndo utamiliki kwa jina la Yesu.
UKIRI:Kwa jina la yesu nakataa kumilikiwa kiakili nakataa kumilikiwa kimawazo nakatakaa kumilikiwa maisha yangu nakataa kutawaliwa na nguvu za giza nakataa kutawaliwa na kila uwepo wa kishetani nakata kila kuifungo kinachomilki maisha yangu kwa jina la yesu kila kinachonizuia nisisonge mbele nanyamazisha kwa jinala yesu roho zote za mashetani zinazozuia wakina dada wasiolewe nazing'oa kwa jina la Yesu.
                                                            PASTOR: BENEDICT KAMZEE





SOMO:KUKATA MKONO WA KICHAWI
PASTOR:BRUNO
Kabla mambo hayajaharibika mwilini ni lazima yawe yameanza kuharibika rohoni,isaya 59:1kila baya linalompata mtu kuna mkono katikati kama ni baya basi ni mkono wa kichawi asubui ya leo tunakata mikono yote ya watu ya kichawi kuharibika kwa ndoa,magonjwa katikati lazima kuna mkono wa mtu
kuna mikono ya kuiba imewekwa kwenye maisha yako kila hela unayopata iwe inapitiliza.
UKIRI:leo tunakata kila mikono ya kichawi inayonyooshwa kwenye ulimwengu wa roho,kila mikono inayooshwa kwenye huduma yako ninaifyeka kwa jina la yesu,mkono wa umaskini naifyeka yote kwa jina la yesu,kila aliyenyoosha mkono kunitenda mabaya naukata kwa jina la yesu.mkono wowote ulinyooshwa kwenye familia tunaifyeka,tunafyeka kwa jina la yesu mkono wa ndugu yeyote mchawi kiongozi mchawi tunafyeka kwa jina la Yesu.

                                                             PASTOR:BRUNO

SOMO:KUWAFEDHEHESHA WATESI
PASTOR:MWANGAZA
FROM:DAR
zaburi 35:1 Bwana atawaaibisha na kuwafedhehesha wanakutafuta wewe na familia yako, wanaoitafuta nafsi yako mana tangu mwanzo Mungu alituumba ili tuishi maisha mazuri ila shetani anakusudi la kubadili mpango wa Mungu kwa kuyafanya maisha yako kuwa mabaya usiweze kumiliki nyumba,pesa afya njema na kazi nzuri.mambo ya nyakati 7:3 wapo watesi wanaoshughulika na maisha yako unatakiwa usilale kesha na kuomba ili uwakimbize watesi wako
UKIRI:Tunasambaratisha mbinu zote za kishetani zinazozoofisha maisha yetu kila mamlaka ya giza tunaziharibu kwa jina la yesu tunaharibu nguvu zote za watesi wetu kwa jina la yesu kila anayetufatilia tunambomoa na kumsambaratisha kwa damu ya mwana kondoo


                                                       PASTOR:MWANGAZA



SOMO:MACHO YA KIMUNGU
PASTOR:JANE BROWN
FROM:DAR
Joshua 5:13 unapoomba unatakiwa uwe na macho mazuri ya kimungu,tunatakiwa kuvua macho ya mazoea kwa watumishi wa Mungu, kwa viongozi ni lazima uvue kwanza ili umiliki baraka za kimungu uwezi kumuona Mungu vizuri kama hujavua mazoea yako mbele za Mungu Yapo mambo mengi yanayoweza kukurudisha nyuma wewe songa mbele ukivaa macho ya kawaida uwezi kuvuka uwezi kumiliki uwezi kutiisha vaa leo macho ya kimungu.
UKIRI:Baba Mungu nakuja mbele zako naomba utusaidie kuvua macho ya kishetani yanayotufanya tunashindwa kupiga hatua kwa jina la yesu naomba kuona yale makusudi ambayo ulipanga niyaone kwa jina la Yesu tusaidie tuweze kutembea kwenye uwepo wako tunahitaji kutembea kwenye kusudi lako tunamuangamiza shetani na wakala wake wote kwa damu ya mwanakondoo.

                                                         PASTOR:JANE BROWN